F Mbwana Samatta afanikiwa suala la Shomari Kapombe | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mbwana Samatta afanikiwa suala la Shomari Kapombe


Nahodha wa timu ya Taifa, Taifa Stars Mbwana Samatta amefanikiwa kuwashawishi TFF  kuwa mchezaji Shomari Kapombe ajumuishwe kwenye zawadi watakazopewa timu hiyo.

Mara baada ya kufuzu AFCON, hapo jana Rais John Magufuli alitoa zawadi ya viwanja wa kwa wachezaji wote wa kikosi hicho.

"Tuwapongeze TFF kwani linamipango na wachezaji wote walioshiriki katika kampeni hii ya kuwania tiketi na kwa heshima yao basi naondoa Twitter yangu iliyopita kwani tayari mipango ipo barabara kwa kila mchezaji aliyeshiriki," amesema Samatta.

Awali Mbwana Samatta alieleza, 'Kama nahodha ningeomba TFF imuangalie Shomari Kapombe katika zawadi ambazo wachezaji watapata, ikishindikana basi wachezaji wote tumchangie kidogo kidogo na endapo vyote visipowezekana, katika ahadi ya Mkuu wa Mkoa nitagawana nae nusu kwa nusu'.