F Kaizer Chiefs yamfukuzia James Kotei | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kaizer Chiefs yamfukuzia James Kotei

Imeripotiwa kuwa miamba wa Afrika Kusini Kaizer Chiefs wapo kwenye mipango ya kumsajili kiungo wa Simba James Kotei ambaye ni raia wa Ghana.

Kwa mujibu wa mtandao wa Ghana Soccernet umesema Kaizer Chiefs wameonesha kuvutiwa na Mghana huyo anayecheza nafasi ya kiungo kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu nchini humo katika msimu wa 2019/20.

Kaizer maarufu kama 'The Amakhosi' wamekuwa wakimfuatilia kwa ukaribu zaidi Kotei ambaye amekuwa ngome imara kwa msimu uliomalizika hivi karibuni kunako Ligi Kuu Bara pamoja na kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wakongwe hao wa Ligi Kuu Afrika Kusini 'PSL' wamemaliza ligi msimu huu wakiwa nafasi ya tisa katika msimamo na wakijikusanyia alama 39.

Kotei ameanza kuvutiwa waya na Kaizer ambaye amekuwa mchezaji bora katika nafasi ya kiungo kwa msimu wa 2018/19.

Mghana huyo mwenye miaka 25, akiwa na Simba amefanikiwa kucheza mechi zote 12 za Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu ambayo waliondolea katika hatua ya robo fainali dhidi ya TP Mazembe ya Congo.

Ofa ya kumsajili mchezaji huyo inatarajiwa kutumwa wiki zijazo za hivi karibuni ili kumaliza mazungumzo na klabu husika ambayo ni Simba tayari kwa kumsajili Kotei.