F Serikali yaja na mfumo mpya wa ajira | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Serikali yaja na mfumo mpya wa ajira


Serikali imewataka waajiri katika Utumishi wa Umma kuhakikisha wanatumia mfumo mpya wa maombi ya kazi ‘Ajira Portal’ uliopo chini ya Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira ili kuondoa changamoto za rushwa na upendeleo wakati wa kuomba au kutoa ajira.

Mfumo huo kwa mujibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni George Mkuchika utakuwa ni muarobaini dhidi ya vitendo vya rushwa,utashi na upendeleo kwa kuwa utakuwa na uwezo wakuchagua waombaji wa ajira kulingana na sifa zao na nafasi walizoomba.