Mchezaji wa Difaa el Jadida ya Morocco, Mtanzania Saimon Msuva amefunguka kuwa kwa msimu ujao anaweza kuondoka ndani ya klabu hiyo na kutimkia barani Ulaya.
Msuva kwa sasa amebakisha mkataba wa mwaka mmoja na Wamorocco hao ambao walimng’oa kutoka Yanga baada ya kufanya vizuri kwa kumaliza mfungaji bora akiwa na mabao 14.
Msuva amesema malengo yake kwa msimu ujao awe Ulaya ambapo anacheza nahodha wa Taifa stars, Mbwana samatta aliye Ubelgiji.
“Naheshimu sana mkataba wangu ambao umebakia ndani ya klabu ya Difaa, lakini wazo langu ni kutoka na kwenda Ulaya. “Unajua nimeshakaa hapo na sasa ni muda wa kuangalia changamoto sehemu nyingine lakini pia kumfuata samatta ambaye anacheza huko.
“Kama itakuja timu ya huko basi lolote linaweza kutokea la mimi kwenda kucheza huko na kuongeza wigo wa wachezaji wanaocheza Ulaya kutokea hapa nchini,” alisema Msuva.