Mbunge wa jimbo la Mtama kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye ameeleza kuguswa na kifo cha aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe.
Robert Mugabe amefariki dunia hii leo akiwa na miaka 95 akiwa nchini Singapore akipokea matibabu kwa muda mrefu sasa.
"Pamoja na mapungufu yake kadhaa kama binadamu, Robert Gabriel Mugabe ni mtoto wa Afrika," ameeleza Nape kupitia mtandao.
Ikumbukwe Mugabe ameiongoza Zimbabwe kutoka 1980 mpaka 2017, alipong'olewa madarakani na makamo wake kwa msaada wa jeshi.