Habari za wakati huu mdau na mfuatiliaji wetu wa blog hii, karibu tena tuangalie faida za baadhi ya vyakula vyetu.
Kwa sasa wacha tuangalie hizi faida za kutumia choroko kiafya;
Kama wewe ni miongoni mwa wale watu wengi ambao hutumia choroko katika mlo wako, basi utakuwa ni miongoni mwa watu wanopata faida za virutubisho hivi vifuatavyo:
Choroko ni kati ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha protini na madini ya phosphorus, calcium , lakini pia choroko husaidia sana kuimarisha mifupa mwilini.
Mbali na hayo, choroko pia husaidia sana kwa afya ya moyo kutokana na mafuta yalipo ndani yake kuwa ni salama, lakini pia husaidia sana katika masuala ya umeng’enywaji wa chakula tumboni.
Pamoja na hayo choroko ina vitamin B1, B2 ambayo husaidia sana kuimarisha mfumo wa fahamu.