F Wanawake acheni kutegemea kuteuliwa Viti Maalum - Diwani | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wanawake acheni kutegemea kuteuliwa Viti Maalum - Diwani


Na Thabit Madai, Zanzibar

Wanawake nchini wametakiwa kujitokeza kuwania nafasi mbali mbali za uongozi katika majimbo ya Uchaguzi na kuacha tabia ya kusubiri kuteuliwa katika nafasi za maalumu.

Wito huo umetolewa na Diwani wa wardi ya Mlandege Jimbo la Malindi,Bi Kinuni Rashid Slim katika Mkutano maalumu wa kushajihisha wanawake kuwania nafasi mbali mbali za Uongozi katika majimbo yao ifikapo mwaka 2020 katika uchaguzi Mkuu.

Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha waandishi wa habari Wanawake Nchini Tamwa ambao ulifanyika  katika Shule ya Mwembe ladu Mjini Unguja.

Diwani kinuni alisema  huu si wakati wa wanawake Nchini kusubiri kuteuliwa katika nafasi maalumu bali ni wakati wa kuanzisha mapambano na kujitokeza katika majimbo na kuchukua nafasi mbali mbali za uongozi.

Aliongeza kusema kuwa ushiriki wa wanawake katika uongozi na vyombo mbali mbali vya kutunga sheria bado ni mdogo.

“Ukweli kuwa wanawake wenzangu bado tupo nyuma sana katika kuwania nafasi mbali mbali za uongozi na kupelekea kuwamuliwa mambo mengi ambayo yanatuhusu sisi” alisema Diwani huyo.

Alieleza kwamba wanawake wanapojitokeza kwa wingi katika kuwania nafasi hizo na kuchaguliwa katika nafasi mbali mbali katikavyomba vya kutoa maamuzi na kutunga sheriahupelekea kuwamua na kupanga mambo yanawahusu  wao wanawake.

“Wakina mama tuna mambo mengi yanayotuhusu sisi, tunapokuwa nyuma na hawa wenzetu wanaendelea ktuweka nyuma na kutuamulia kwa kila jambo haya yanayotuhusu sisi wenyewe” alieleza Diwani huyo.

Hata hivyo aliwataka wanawake hao kuwaunga mkono wanawake wenzao ambao wataonesha nia ya kutaka kugombea katika uchaguzi Mkuu.

Aliwaambia kuwa wanawake huwa wanatabia ya wao wenyewe kurudishana nyuma kwa kutukuwa na umoja pindi mwenzao anapokuwa katika king’anyiro cha kuwania nafasi mbali mbali za Uongozi.

Nae Sheikh Ismail Asa kher aliwataka wanawake hao kuwa mstari wa mbele kugombea nafasi za uongozi huku akiwatoa hofu kuwa dini ya kiislamu si kikwazo kwa mwanamke kuwa kiongozi.

“Dini yetu ya kiislamu haiweki kikwazo kwa wanawake kushika nafasi zauongozi hivyo niwatoe wasi wasi  kuwa Dini yetu ipo na miongozo yake na hakuna sehemu iliyokataza wanawake kuwa viongozi” alieleza Sheikh huyo.

Katika mkutano huo wanawake waliojitokeza walikiri kuwa walikuwa nyuma katika uwania nafasi za uongozi na kuahidi kujitokeza katika kushika nafasi mbali mbali ifikapo 2020.

Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Nchini kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa Maendeleo wanaendesha kampeni maalumu ya kuwashajihisha wanawake kuwania nafasi za uongozi ifikapo 2020 katika Uchaguzi Mkuu.