Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Madeni amekabidhi madawati na Meza 3900 kwa Afisa Elimu Sekondari wa jiji hilo kwa ajili ya wanafunzi wapya wanaoijunga na elimu ya sekondari mwaka 2020 lengo ikiwa ni kuondokana na tatizo la uhaba wa madawati na meza.
Akikabidhi madawati hayo ,Dr.Madeni amesema kuwa jiji la Arusha limetumia kiasi cha shilingi milioni 105 kutengeneza madawati 3900 ambayo yametengenezwa na Kituo cha Ufundi Kaloleni ambacho kipo chini ya shule ya msingi kaloleni hivyo kuokoa kiasi cha shilingi milioni 200 ambazo zingetumika kwa wakandarasi wa makampuni binafsi.
Dr,Madeni amesema kuwa jiji hilo limekua kiasi hicho cha fedha baada ya kutumia Kituo hichoi cha ufundi kinachomilikia na serikali ambapo wamejirisha na ubora wa hali ya juu wa madawati hayo ukilinganisha nay ale yanayotengenezwa na Wakandarasi wa makampuni binafsi.
“Fedha hizi tulizoziokoa zinaweza kuelekezwa kwenye matumizi mengine ikiwemo ujenzi wa madarasa mapya ili kuendelea kuboresha elimu” Alisema Dr.Madeni.
Aidha amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro kwa kusimamia vyema Halmashauri na kufanikisha kazi hiyo kubwa na pia amemshukuru Raisi John Pombe Magufuli kwa juhudi zake katika kuboresha sekta ya elimu ambayo ni sekta muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Afisa Elimu Jiji la Arusha Valentine Makuka amesema kuwa madawati hayo yataziba pengo la uhaba wa madawati hususan kwa wanafunzi wapya wanaojiunga na kidato cha kwanza mewakani hivyo kusaidia kukuza taalumu na kuinua kiwango cha ufaulu.
Amesema kuwa maboresho hayo ya kupata madawati bora yameenda sambamba na ujenzi wa madarasa mapya ambapo hakuna mwanafunzi atakayekosa darasa au dawati kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Raisi Magufuli,Mkuu wa Wilaya ya Arusha na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha.