Mwanadada kutoka nchi Tanzania Jacqueline Mengi ameibuka kinara baada ya kutajwa katika mtandao wa masuala ya mitindo na urembo wa nchini Nigeria, stylerave umetoa orodha ya wanawake 30 warembo zaidi wa Afrika nayeye ndio ameongoza.
Mrembo huyo ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2000, katika tovuti hiyo ametajwa kutokana na kujishughulisha kwake na biashara ya samani za majumbani kupitia brand yake ya Molocaho ambapo kwa sasa inafanya vizuri Afrika Mashariki na Afrika.
Pia ametajwa kutokana na kutoa misaada kwaajili ya watoto wadogo wa shule za msingi kupitia taasisi yake ya Dr Ntuyabaliwe Foundation ambayo imekuwa mchango mkubwa wa kujenga maktaba za watoto pamoja na vifaa mbalimbali vya shule pamoja na kukarabati miundombinu ya shule.
“Truly an honor to not only be on top of this list but to be among these beautiful and accomplished women. Congratulations to all of you on the list and thank you @stylerave_ for recognizing us all,” Jacqueline Mengi shukrani kwa mtandao huo.
Pia katika list hiyo pia ametajwa DC wa Kisarawe Jokate Mwegelo ambaye ameonekana akipambana katika harakati ya kumkomboa mtoto wa kike kupitia elimu.