F Viongozi wa CHADEMA kanda ya ziwa watiwa mbaroni Magu . | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Viongozi wa CHADEMA kanda ya ziwa watiwa mbaroni Magu .


Wakati Taifa likipambana na maambukizi ya Virusi vya Corona, Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza, imewatia mbaroni viongozi wa kanda ya Ziwa ishirini na wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa kukiuka maagizo ya serikali.

Kamati hiyo imewatia mbaroni viongozi hao na wanachama wa chama hicho, kwa tuhuma ya kufanya mikusanyiko ya kuendesha vikao vya ndani, vinavyoweza kusababisha kuenea Virusi hivyo, vinavyosababisha ugonjwa wa Covid 19.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Magu Dkt. Philemon Sengati, ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo amesema vitendo hivyo havitavumilika.