Ndizi ni moja ya chakula kinachopendwa sana na watu wengi, lakini kwa hapa nchini chakula hiki huongoza kwa kuliwa zaidi na watu wa kabila la Wahaya kutoka mkoa wa Kagera, Bukoba. Sasa leo katika mapishi tutaandaa ndizi mchemsho twende sote...
MAHITAJI
Nyama robo
Ndizi mzuzu mbichi 5 au kulingana na ukubwa wa familia yako
Vitunguu maji
Giligiliani vijani kiasi
Vitunguu swaumu
Rosemary (vijani vichache)
Bay (vijani kiasi)
Karoti
Chumvi
Oliver oil kijiko cha mezani kimoja
Black pepper
Chills endapo unapenda
Namna ya kuandaa
Menya ndizi zako na uzioshe vizuri kwa maji safi na salama.
Katakata vitunguu maji, na karoti kwa mtindo uupendao
Jinsi ya kupika
Chemsha nyama na ikiashaiva vizuri weka chumvi kiasi, bay, rosemary, black paper vyote hivi utaweka wakati nyama ikiendelea kuchemka.
Nyama ikishaiva vizuri weka vitunguu maji na vitunguu swaumu pamoja na nndizi kisha acha viive vyote kwa pamoja, lakini kabla ya kutoa weka karoti.
Baada ya dakika 5 unaweza kutoa chakula motoni na kitakuwa ni tayari kimeiva na unaweza kula mchana au usiku pia.
0 Comments