F Watu wasiopungua 50 wafariki katika mgodi ulioporomoka Mashariki mwa Congo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Watu wasiopungua 50 wafariki katika mgodi ulioporomoka Mashariki mwa Congo

Shirika moja lisilo la kiserikali la uchimbaji madini nchini Congo, limesema kuwa watu wasiopungua 50 wanahofiwa kufariki wakati mgodi mmoja wa dhahabu ulipoporomoka karibu na mji wa Kamituga Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hapo jana.

Rais wa Mpango wa Msaada na usimamizi wa kijamii wa wanawake Emiliane Itongwa, amesema kuwa kisa hicho kilitokea katika eneo la mgodi wa chumvi katika saa za alasiri kufuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha katika eneo hilo.Itongwa ameongeza kuwa wachimbaji migodi kadhaa walikuwa kwenye shimo ambalo lilikuwa limefunikwa na hakuna mtu angeweza kutoka nje.

Ajali za uchimbaji madini katika migodi ambayo haijadhibitiwa nchini Congo ni matukio ya kawaida huku vifo vya mamia ya watu kila mwaka vikitokea katika migodi ambayo wachimbaji walio na vifaa duni huchimba kina kirefu chini ya ardhi kutafuta madini.