Ndege mbili za kivita aina ya F-5E zinazomilikiwa na Kikosi cha Anga cha Taiwan, ziligongana angani karibu na wilaya ya Pingtung na kudondoka baharini.
Imeripotiwa kuwa ndege nne aina ya F-5E ziliondoka kutoka kambi ya Taitung Zhi-Hang Air Base kwa ajili ya mafunzo, ambapo mbili ziligongana angani, na marubani wa ndege hizo walifanikiwa kujirusha.
Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa (MND) ilitangaza kwamba helikopta za jeshi na boti za doria zilipelekwa katika eneo ambalo ajali ilitokea.
Timu za wazima moto kutoka Taitung na Pingtung pia zilipelekwa katika eneo hilo kwa ajili ya shughuli ya utafutaji eneo la pwani.
0 Comments