F Steve Nyerere amuomba Waziri kuingilia kati changamoto ya bando | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Steve Nyerere amuomba Waziri kuingilia kati changamoto ya bando


Msanii wa filamu Steve Nyerere amemuomba Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Faustine Ndugulile kuingilia kati na kutoa japo neno moja kuhusu changamoto iliyokuwepo kwenye mitandao ya simu hasa upande wa vifurushi.

Kupitia ujumbe wa Steve Nyerere aliomuandikia Waziri huyo kupitia mtandao wa Instagram unaeleza kuwa 

"Mhe Waziri nakuomba sema neno 1 tu kwenye suala la bando na vifurushi, hili ni janga na msiba wa wanyonge wanalia kila kona, najua unajua kwani Serikali haijawahi kushindwa kitu kwa kusimama na wananchi wao, ipo tija ya haraka sana kukaa kikao na haya makampuni" 

"Pasaka hii inatufika tukiwa hoi na bando tu mengine yote Bye, Mhe Waziri ni kilio cha wapiga kura wetu lakini tusisahau sasa hivi dunia imebadilika kila jambo lipo kwenye simu na taarifa zote mitandaoni sasa kwa bando, hili tunahitaji huruma yako mzee mwenzangu embu simama sema na Watanzania kuhusu bando, nakuamini sana" ameongeza Steve Nyerere 

Siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la gharama na upinguzwaji wa aina ya vifurushi kwa makampuni ya mitandao ya simu hali ambayo inaleta shida kwa watumiaji hapa nchini.

Post a Comment

0 Comments