Leo kuanzia Saa 2:00 usiku jiji litasimama kwa muda, mtanzania Hassan Mwakinyo akienda kuvunja rekodi kwenye pambano la Rumble in Dar.
Pambano hilo litapigwa kwenye ukumbi wa Next Door Arena, Masaki likitanguliwa na mapambano mengine sita.
Hassan Mwakinyo bondia namba moja nchini mbali na kuwania ubingwa wa Afrika (ABU), endapo atamchapa Anthony Mayala ataweka rekodi ya kuwa bondia wa kwanza kumchapa Muangola huyo.
0 Comments