Na John Walter-Manyara.
Kilele cha maazimisho ya Siku ya wauguzi duniani Kitaifa inafanyika mjini Babati leo mei 12,2021 katika mkoa wa Manyara ikiongozwa na kauli mbiu isemayo "Wauguzi sauti inayoongoza dira ya huduma ya afya".
Mgeni rasmi ni waziri wa ofisi ya rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu.
Haya ni maneno yaliyoandikwa katika baadhi ya Mabango mbalimbali ya wauguzi.
Wauguzi walio kwenye mazingira magumu ya Kazi wapewe makazi.
Ushirikishwaji katika maamuzi kiutawala na kisera kwa wauguzi.
Wauguzi viongozi wapewe mafungu ya fedha kuratibu huduma za uuguzi.
Wauguzi wawe sehemu ya maamuzi ya kiutawala na kisera katika ngazi zote.
0 Comments