Iran na nchi nyingine sita zenye nguvu zaidi ulimwenguni, zimeahirisha mazungumzo yao kuhusu mkataba wa nyuklia, ili kuruhusu mashauriano binafsi kufanyika katika nchi zao.Mjumbe wa Umoja wa Ulaya katika mazungumzo hayo Enrique Mora amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari.Hakueleza ni lini mazungumzo hayo yatarejea tena.
Hata hivyo amedokeza kwamba hatua kubwa zimepigwa na washiriki watakuwa na taswira kamili kuhusu namna walivyokaribu kukubaliana watakaporejea katika mazungumzo.Mora ameongeza kuwa anatarajia shirika la Umoja wa Mataifa ya kudhibiti matumizi ya nishati ya atomiki pamoja na Iran, zitakubaliana kurefusha muda wa kuchunguza vinu vya Iran. Muda wa shirika hilo unakamilika Juni 24.
Balozi wa Urusi katika mazungumzo hayo Mikhael Ulyanov pia aliwaambia wanahabari kwamba hakuna ajuaye lini mazungumzo hayo yataanza tena.
0 Comments