F Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara akutana na watumishi wa Wizara hiyo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara akutana na watumishi wa Wizara hiyo


Na Maridhia Ngemela Mwanza

 Waziri wa u ujenzi na uchukuzi Mwita Waitara amewataka watumishi wa wizara hiyo kuwa na mawasiliano ili kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi zaidi .

Katika kuimarisha utendaji kazi wenye tija kwa Jamii na Serikali,mhe.Mwita Waitara amekutana na watumishi wa Wizara hiyo kwa lengo la kuangalia utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hizo.

Katika kikao hicho,Waitara aliipata nafasi ya kupokea taarifa mbalimbali za utekelezaji kutoka katika Taasisi ambazo ziko chini yake.

Aidha, Waitara aliwasisitiza watumishi waendelee kufanya kazi kwa weledi na ubunifu ili kuiwezesha Serikali kupata mapato ambayo yatasaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali hapa Nchini.

Waitara alisema kuwa atakuwa bega kwa bega na Kila Taasisi ili waweze  kujadiliana kwa kina juu ya utekelezaji wa majukumu, changamoto,mafanikio na mikakati itakayosaidia Wizara kusonga mbele na kufikia malengo.

Kwaupande wake Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Kampuni ya huduma za Meli(MSCL) Philemon Bagambilana alisema kuwa wanaendelea na kazi ya uendeshaji wa Meli za Serikali katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa lengo Kuu ikiwa ni kutoa huduma kwa Watanzania.

"Ziwa Victoria tuna Meli Tisa, Tanganyika tuna Meli tatu na boti moja na Ziwa Nyasa tuna Meli 2  miongoni mwa Meli hizo Kuna ambazo ziko kwenye ukarabati",alisema Bagambilana

Nae Kaimu Meneja wa Tanroad Mkoani Hapa Vedastus Maribe alisema kuwa wanaendelea kushirikiana na Wizara kutekeleza miradi iliyopo kwa ufanisi mkubwa ili iweze kukamilika kwa wakati likiwemo daraja la Kigongo-Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2 litakalogharimu sh582 bilion.

Post a Comment

0 Comments